Jinsi Ya KUJITAMBULISHA DM Au Kwenye Text Kwa Mara Ya Kwanza Unapomtafuta Mtu Yoyote.
M4A•Jakson koti
Manage episode 406395894 series 3280689
Sisällön tarjoaa Innocent Ngaoh. Innocent Ngaoh tai sen podcast-alustan kumppani lataa ja toimittaa kaiken podcast-sisällön, mukaan lukien jaksot, grafiikat ja podcast-kuvaukset. Jos uskot jonkun käyttävän tekijänoikeudella suojattua teostasi ilman lupaasi, voit seurata tässä https://fi.player.fm/legal kuvattua prosessia.
Kama wewe ni wale ambao unawatumia watu DM au text za kawaida Kwa Mara ya Kwanza kama vile "Niaje, Mambo, Vipi, Shwari Mkuu, Harakati Ni Vipi Kiongozi, Mrembo mambo n.k" Tambua unakosea sana Tena sana hiyo siyo Kujitambulisha badala ni salamu tu. Swali linakuja unajua jinsi ya Kujitambulisha mtu akiona DM au text Yako apate kuijibu bila kupuuzia. Unahitaji kuzingatia maeneo matano wakati unamuandika Mtu DM Yako; 1. Jina la mtu unayemtumia ujumbe wako. 2. Jina lako. 3. Shughuli Yako. 4. Hitaji au shida Yako. 5. Hitimisho. Ukizingatia mambo yote hayo DM zako zitajibiwa mpaka ushangae. Kwa mfano... "Habari kaka Amos Nyanda naitwa Innocent Ngaoh ni Mwandishi wa Vitabu pia ni mtengeneza maudhui ya mtandaoni ya kuelimisha jamii, nilikuwa naomba usaidizi ni wapi nitapata ujuzi wa copywriting Ili niwe Mwandishi mzuri wa Malala na Vitabu. Natanguliza shukurani." Mfano wa DM hiyo akiona tu lazima atajibu, Kwa sababu Iko straight to the point. Kujitambulisha ni Sanaa. Ndiyo maana... Una dakika nane za kujua Namna Rahisi ya Kujitambulisha Ili uwe GURU yaani gwiji. Chukua hatua Sasa.
…
continue reading
111 jaksoa