Jinsi Ya Kuonyesha Kipaji Chako Hadi Kukupa Matokeo Makubwa...!
M4A•Jakson koti
Manage episode 375351214 series 3280689
Sisällön tarjoaa Innocent Ngaoh. Innocent Ngaoh tai sen podcast-alustan kumppani lataa ja toimittaa kaiken podcast-sisällön, mukaan lukien jaksot, grafiikat ja podcast-kuvaukset. Jos uskot jonkun käyttävän tekijänoikeudella suojattua teostasi ilman lupaasi, voit seurata tässä https://fi.player.fm/legal kuvattua prosessia.
Hivi unakijua kipaji chako au kikubwa ni uhai? Pasipo kujali unajua au hujui kipaji chako ila tambua una zawadi ya kipaji ambayo ulipewa na Mungu hata kabla ya kuzaliwa kwako. Kwahiyo... Kuzaliwa kwako Ina maana una kipaji ndani yako. Swali la kujiuliza. Je, unakijua kipaji chako? Hongera kwa kujua kipaji chako cha .... (Taja kimoyomoyo) Ina maana tayari umeshajua kusudi la kuzaliwa kwako. KIPAJI = KUSUDI. Lakini... Kujua kipaji chako haitoshi ni lazima uonyeshe kipaji chako kwa ulimwengu yaani dunia itambue na kunufaika na kipaji chako. Kwa sababu... Kipaji siyo kwa ajili yako bali ni kwajili ya kuwatumikia wengine. Unajiuliza ni kwa namna gani si ndiyo? Ni hivi... Milliard Ayo ana Kipaji cha utangazaji ila wananifaika na kipaji chake ni wasikilizaji wake si ndiyo eeh! Samatta ana kipaji cha kucheza mpira ila wanufaika ni mashabiki na wapenzi wa mpira wa kufunga magoli na namna anavyochezea mpira. Masoud Kipanya ana kipaji cha kuchora ila wanunuifa na michoro ni watazamaji wa michoro yake si ndiyo eeh! Joel Nanauka ni mwandishi wa vitabu ila wanuafaika na uandishi wa vitabu vyake ni wasomaji wa vitabu vyake. Kuna mifano mingi kuhusu watu wenye vipaji ambao walithubutu kuonyesha vipaji vyako, ni wewe Kuthubutu sasa kuonyesha kipaji chako. Kwahiyo... Kadiri unavyoonyesha kipaji chako ndivyo unaongeza nafasi ya kufanikiwa kupitia kipaji chako. Kumbuka Mafanikio ya kipaji chako si tukio la usiku mmoja ni mchakato. Je, unaanza lini kuonyesha kipaji chako kwenye ulimwengu? Usiogope kuonyesha Kipaji chako. Mwisho kabisa... Ni vema ukajua faida za kuonyesha kipaji chako kwa wewe kuniambia hapa chini comment ili tujifunze kwa pamoja. Kauli Mbiu: “Maisha Ni Kuthubutu”
…
continue reading
111 jaksoa