UK's experience na Dada lao!: What to expect while studying in the UK (From a Tanzanian who graduate in UK)
Manage episode 347177507 series 3405885
Ukitaja nchi zenye elimu bora, ni-imani yangu Uingereza nayo itawemo. Hii ni kutokana na kuwa na vyuo vizuri na watu wenye “background” tofauti tofauti, inayomfanya mwanafunzi anaeenda kusoma huku apate kujifunza na kupata “exposure” ya kutosha, hayo ndo maoni yangu juu ya kwenda kusoma Uingereza
Kwenye “episode” hii tumeweza kupata maoni mengine juu ya kusoma Uingereza kutoka kwa Faith. Ambaye yeye ni mwanafunzi nchini humo kwa miaka mitatu sasa, kuachilia mbali maoni yake juu ya kusoma huko, ametueleza pia ni vitu gani vya kuzingatia kuazia unapoanza ku-apply visa mpaka kufika nchini humo.
Faith pia ametuakikishia usalama wa nchini humo ni mzuri na kutuelezea pia kuhusu mfumo mzima wa kupata matibabu ukiwa nchini humo kama mwanafunzi. Mbali na kuiongelea Uingereza Faith pia ametuelezea na kutupa ushauri sisi kama wanachuo kutoka sehemu yeyote na kutuelezea umuhimu wa kujichanganya na kujitoa kwenye “activities” tofauti tofauti vyuoni.
34 jaksoa